Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burkina Faso kumzika upya Sankara

Burkina Faso Kumzika Upya Sankara Burkina Faso kumzika upya Sankara

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Serikali ya kijeshi ya Burkina Faso inajiandaa kuzika masalia ya mwili wa rais wa zamani wa nchi hiyo Thomas Sankara hii leo Alhamisi, huu familia yake ikikataa kushiriki mazishi hayo.

Shughuli ya mazishi yake imepangwa kufanyika katika eneo alilopigwa risasi Bw Sankara pamoja na watu wengine 12 katika siku ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 1987.

Familia yake inasema inaweza kutoshiriki mazishi hayo kwasababu haufurahishwi na eneo anakotakiwa kuzikwa, lakini serikali inasema kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kulingana na sheria, ya "utengamani na haki, usalama na pia kwa faida za nchi".

Sankara bado ni shujaa kwa wengi barani Afrika kutokana na msimamo wake kuhusu nchi yake namataifa mengine pamoja na maisha yake kwa ujumla.

Sankara alichukua mamlaka ya nchi ya Burkinafaso kama rais mwaka 1983, akauawa baada ya miaka minne mamlakani akiwa na umri wa miaka 37, katika mapinduzi ya kijeshi yaliyotekelezwa na rafiki yakewa karibu Blaise Compaore.

Compaore alichukua hatamu za uongozina kuiongoza burkinafaso kwa miaka 27, kabla ya kung’olewa mamlakani mwaka 2014 kufuatia maandamano ya raia dhidi ya uongozi wake.

Sankara alighukumiwa kifungo chya maisha mwaka 2022, akiwa hayupo nchini baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya Sankara.

Chanzo: Bbc