Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burkina Faso: Watu 170 wameuawa na wanajihadi

Burkina Faso Magaidiii 53 Burkina Faso: Watu 170 wameuawa na wanajihadi

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waendesha mashtaka nchini Burkina Faso, wamesema karibia watu 170 wameuawa katika mashambulio kwenye vijiji vitatu kaskazini mwa nchi hiyo wiki moja iliyopita, wanajihadi wa kiislamu wakinyooshewa kidole.

Kwa mujibu wa waendesha mashtaka, siku hiyo hiyo, Februari 25 katika mashambilio tofauti, wanajihadi hao walishambulia msikiti magharibi mwa nchi hiyo na kanisa moja kaskazini mwa burkina Faso, ambako dazeni ya watu waliuawa.

Mamlaka zinasema vijiji vilivyolengwa ni pamoja na Komsilga, Nodini na Soroe jimboni Yatenga, ambapo pamoja na kuua, walijeruhi watu, kuchoma nyumba moto na kuharibu miundombinu mingine.

Tayari wizara ya mambo ya ndani imeagiza uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo, watu walionusurika wakisema miongoni mwa waliouawa ni pamoja na wanawake na watoto.

Mashambulio ya wanajihadi yamesababisha vifo vya takriban watu elfu 20 na wengine zaidi ya milioni 2 kuhama makazi yao katika moja ya nchi maskini zaidi duniani iliyoko Sahel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live