Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burkina Faso: Serikali yavifungia vyombo vitano vya habari

 Press Media Conference Microphones 13298230 Detail Burkina Faso: Serikali yavifungia vyombo vitano vya habari

Mon, 29 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Juu la Mawasiliano nchini Burkina Faso (CSC) linaendelea kuviwekea vikwazo vyombo vya habari ambavyo vilitaja ripoti ya Human Rights Watch ambayo inalishutumu jeshi kwa kuua zaidi ya raia 220 katika vijiji viwili mwezi wa Februari mwaka huu.

CSC imeamua kusimamisha matangazo ya kituo cha televisheni ya TV5 Monde kwa wiki mbili, na kuzuia ufikiaji wa tovuti yake na vile vile tovuti za vyombo vingine sita vya habari: magazeti ya Ufaransa "Ouest France" na "Le Monde", Gazeti la kila siku la Uingereza "The Guardian" , idhaa ya Ujerumani Deutsche Welle, shirika la habari la Senegal la APAnews na wshirika la habari la EcoFin lenye makao yake nchini Cameroon na Uswisi.

Vyombo hivi vya habari vinashutumiwa kwa kuchapisha "taarifa za kijasusi na zenye mwelekeo" dhidi ya jeshi. Mwishoni mwa juma lililopita, BBC na Sauti ya Amerika zilifungiwa matangazo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, CSC "inaalika vyombo vyote vya habari kuacha kusambaza" maudhui haya, chini ya adhabu ya vikwazo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live