Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burkina Faso, Mali na Niger zaafiki mradi wa muungano

Mali, Burkina Faso Na Niger Wajiondoa Kwenye ECOWAS Burkina Faso, Mali na Niger zaafiki mradi wa muungano

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mawaziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso, Mali, na Niger, Karamoko Jean Marie Traore, Abdoulaye Diop, na Bakary Yaou Sangare, wameidhinisha rasimu ya waraka wa kuundwa muungano wa nchi hizo tatu wakati wa mkutano katika mji mkuu wa Niamey.

Rasimu hiyo sasa lazima isainiwe na viongozi wa nchi hizo tatu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali Abdoulaye Diop amenukuliwa na Shirika la Habari la Sputnik akisema kwamba nchi hizo zinataka kufanya kazi pamoja.

Ameongeza kuwa tamko ambalo lilipitishwa na mataifa hayo matatu limenuia kubainisha kuwa tangazo la kujiondoa kutoka ECOWAS, "lazima kuchukuliwe kwa uzito zaidi."

Mnamo Septemba 2023, viongozi wa kijeshi wa Mali, Burkina Faso na Niger walitia saini mkataba wa Waitifaki wa Nchi za Sahel (AES) ili kuunda mfumo wa pamoja wa ulinzi baada ya kuzorota uhusiano na Ufaransa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kufuatia mapinduzi ya kijeshi katika nchi hizo.

Mwishoni mwa Januari, mataifa ya Waitifaki wa Nchi za Sahel yalitangaza kujiondoa kutoka ECOWAS, yakitaja kutofanikiwa shirika hilo katika kupambana na ugaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live