Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burkina Faso: Kiongozi wa kijeshi akutana na rais aliyepinduliwa

BurkanaFaso Kukutana Burkina Faso: Kiongozi wa kijeshi akutana na rais aliyepinduliwa

Wed, 22 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali ya kushangaza kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso amekutana na rais aliyempindua katika mapinduzi Januari iliyopita. Roch Marc Christian Kabore aliandamana na rais mwingine wa zamani Jean-Baptiste Ouedraogo.

Maafisa walisema mkutano huo ulionyesha hamu ya Luteni Kanali Paul-Henri Damiba ya kutaka maridhiano na kwamba hali ya usalama wa nchi ilijadiliwa.

Video ya mkutano huo inaonyesha wawili hao wakisaliamana na hata kutabasamu huku kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso akimkaribisha mtu aliyemtoa madarakani kwa matembezi kwenye zulia jekundu mahali anapopafahamu vyema - ikulu ya rais. Taarifa ilisema Roch Marc Christian Kabore alikuwepo kujadili masuala ya usalama na kujaribu kutuliza joto la kisiasa.

Mnano mwezi Januari Luteni Kanali Paul-Henri Damiba alisema alimuondoa madarakani rais Kabore kwa sababu alishindwa kuzuia mashambulizi ya wapiganaji wa kijihadi. Licha ya ahadi ya kuimarisha usalama, ghasia zimeendelea. Kiongozi huyo wa kijeshi pia ametangaza kwa utata kipindi cha mpito cha miaka mitatu kabla ya uchaguzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live