Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge lamkataa Waziri Mkuu DRC

3efc8a1a0de0a57bf4abd0a8e23082c4.jpeg Bunge lamkataa Waziri Mkuu DRC

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Wabunge nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) jana wamepiga kura kumuondoa madarakani Waziri Mkuu, Sylvestre Ilunga Ilukamba.

Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ikiwemo BBC na ‘The East African’, Ilukamba amepewa masaa 24 kujiuzulu.

Imeelezwa kuwa wakati kura za kutokuwa na imani naye zikipigwa, waziri huyo hakuwepo. Mtandao wa ‘The East African’ umeripoti kuwa kura za ndio zilikuwa 367 na hapana zilikuwa saba.

Aidha, vyanzo vimeeleza kuwa wabunge wanamshutumu Ilukamba, Rais wa zamani wa nchi hiyo, Joseph Kabila aliyeiongoza kwa miaka 18 (2001-2019), na mawaziri wake kwa utendaji kazi mbovu.

Tukio hili linatajwa kuwa la kwanza DRC tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1960.

Chanzo: habarileo.co.tz