Bunge la nchini Pakistan hii leo limemchagua waziri mkuu mpya baada waziri alliyekua madarakani kupigiwa kura ya kutokua na imani nae. Bw. Imran Khan alikumbana na kura hiyo iliyomwondoa kabisa kwenye nafasi yake ya uwaziri mkuu saa za mapema siku ya jana.
Shahbaz Sharif ambaye ni kiongozi wa muungano wa upinzani nchini humo , ambaye alihusika kwa kiasi kikubwa kuchochea kutokua na imani na Bw. Khan , anatarajiwa kushinda kwa kura nyingi.
Bw. Khan mwenye umri wa miaka 69, alijaribu mara kadhaa kuzuia mipango ya upigwaji kura ya kutokua na imani nae kwa kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi wa haraka haraka .
Licha ya kwenda mahakama ya juu nchini humo , ombi lake lilikataliwa na mahakama ikasema kuwa maombi yake hayana nafasi kikatiba na kwamba kura ya kutokua na imani nae iendelee
Hata hivyo Bw. Imran Khan ambaye wafuasi wake wameadamana kwenye viunga vya miji ya Pakstan baada ya kutenguliwa, anailaumu jumuiya ya kimataifa kwa kuondolewa kwake madarakani
Bila kutoa ushahidi, amelalamika kuwa mahasimu wake waliungana na Marekani kumuondoa madarakani kutokana na sera yake ya mambo ya nje juu ya Afghanistan, Russia na China., amdai ambayo Washington imeyakanusha.