Bunge la nchini Benini limepiga kura kupitisha Sheria mpya inayoruhusu utoaji wa mimba nchini humo mara baada ya kuidhinishwa kwa sheria hiyo ya muda mrefu.
Kupitia sheria hiyo iliyopitishwa Oktoba 13, 2021 wanawake nchini humo wataruhusiwa kutoa ujauzito endapo utakuwa na madhara makubwa katika maisha ya mama hasa kwenye elimu, kazi, biashara na sehemu zinginezo.
Hapo awali wanawake nchini humo waliruhusiwa kutoa ujauzito pale tu wataalamu wa afya walipothibitisha kuwa ujauzito huo unatishia uhai wa mama na mtoto.
Inaelezwa kuwa mjadala huo ulipinga vikali na baadhi ya wabunge wa bunge hilo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu hata hivyo mapingamizi hayo yaligonga mwamba.