Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge la Uganda kupitisha mswada muhimu wa bomba la mafuta

44e968203e95e86c80e7fc7db752ab6b Bunge la Uganda kupitisha mswada muhimu wa bomba la mafuta

Sun, 28 Nov 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Bunge la Uganda linatarajia kupitisha mswada wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (Masharti Maalumu), 2021 siku ya Jumanne (Novemba 30) ili kuruhusu uendelezaji na utekelezaji wa mradi unaosubiriwa kwa hamu kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini, Dk Ruth Nankabirwa Ssentamu amesema Jumapili wakati wa Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uganda lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam kuwa "baada ya muswada huo kusainiwa tutaona shughuli nyingi."

Marais wawili, Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda walihudhuria kongamano hilo.

"Napenda kumshukuru Rais wa Tanzania (Samia Suluhu Hassan) kwa kufuatilia na kupitisha sheria ya utekelezaji," alisema.

"Wawekezaji wamekuwa wakisubiri sheria ya utekelezaji, ambayo ni muhimu sana kwa mradi.

Ninataka kuwahakikishia kuwa nchini Uganda, mswada wa bomba la mafuta ghafi wa Afrika Mashariki utahitimishwa na bunge siku ya Jumanne,” alisisitiza.

Sheria hiyo ni hitaji chini ya Makubaliano ya Kiserikali ya Uganda na Tanzania yaliyotiwa saini sambamba na Makubaliano ya Serikali Mwenyeji kwa mradi huo.

Muswada huo utawezesha baadhi ya vifungu vya Mkataba wa Kiserikali uliotiwa saini kati ya Uganda na Tanzania pamoja na Mkataba wa Serikali mwenyeji uliosainiwa kati ya Uganda na Kampuni ya Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki ili kuruhusu maendeleo ya mradi huo.

Kwa haraka Waziri alibainisha kwamba wakati wa utekelezaji wa mradi, wawekezaji wanapaswa kufanya ubia na kwamba kampuni ya Tanzania au Uganda kwa upande wowote haitachukuliwa kuwa kampuni ya kigeni.

Eacop ni bomba lenye joto la kilomita 1,445, sehemu muhimu ya uuzaji wa mafuta ya Uganda, ambayo yatasafirisha mafuta ghafi kutoka maeneo ya uzalishaji wa mafuta ya Ziwa Albert katika miradi ya Tilenga na Kingfisher magharibi mwa Uganda hadi Tanga nchini Tanzania.

Chanzo: www.habarileo.co.tz