Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge la Senegal lapasisha uamuzi wa kuahirishwa uchaguzi wa rais

Senegal Polisiiiiiii Bunge la Senegal lapasisha uamuzi wa kuahirishwa uchaguzi wa rais

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bunge la Senegal limepasisha muswada wa kuahirisha uchaguzi wa rais hadi Disemba 15 mwaka huu wa 2024 na kuongeza mauda wa rais anayemaliza muda wake, Macky Sall. Hatua hiyo iliyochukuliwa jana jioni imezua vurugu na ghasia ndani ya Bunge la Senegal mjini Dakar.

Maafisa wa polisi walilazimika kuingilia kati kuamulia mvutano huo na kuwatoa nje wabunge wa upinzani, ambao walipinga kuahirishwa zoezi la uchaguzi wa rais na pia kuongezwa mauda wa utawala wa Macky Sall.

Jumapili iliyopita wafuasi wa vyama vya upinzani walikabiliana na polisi katika mji mkuu wa Senegal, Dakar baada ya Rais Macky Sall kutangaza habari ya kuakhirisha kwa muda usiojulikana uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Februari 25, na hivyo kuzusha wasiwasi kimataifa.

Siku moja tu kabla ya kuanza kwa kampeni rasmi, Rais Sall alilitumbukiza taifa kwenye hatima isiyojulikana, alipotangaza kuwa ameamua kuingilia kati kwa sababu ya mzozo uliopo kati ya Bunge na Mahakama ya Katiba kuhusu kukataliwa kwa baadhi ya wagombea. Dakar, Senegal

Wakati huo huo Umoja wa Afrika (AU) umetangaza kuwa unatiwa wasiwasi na hatua ya serikali ya Senegal ya kuakhirisha uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.

Katika taarifa yake, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat ameitolea wito serikali ya Senegal kuendesha zoezi la uchaguzi huo kwa amani, uwazi na kwa mujibu wa maelewano ya kitaifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live