Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge la Libya laipinga Israel

Israel Colombiaaa Bunge la Libya laipinga Israel

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Bunge la Libya jana Jmatatu alieleza kuwa wawakilishi wa bunge hilo kwa kauli moja walipiga kura ya kujinaisha kuhusisha uhusiano na utawala wa Kizayuni.

Kura hizo zilipigwa na wabunge wa Libya katika kikao chao cha karibuni katika makao makuu ya bunge hilo huko Benghazi. Msemaji wa Bunge la Libya amefafanua kwa kusema bunge kwa kauli moja imeidhinisha sheria ambayo inajinaisha kuhusisha uhusiano na Israel.

Wito wa kujinaisha kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni umetolewa tangu Eli Cohen, Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Kizayuni alipotangaza mwezi uliopita kukutana na mwenzake wa Libya, Najla Al-Mangoush.

Baada ya kufichuliwa mazungumzo ya pande mbili hizo, maandamano mengi yalishuhudiwa katika miji mbalimbali ya Libya kulalamikia mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Libya na utawala wa Kizayuni; ambapo waandamanaji walichoma moto bendera za utawala wa Kizayuni. Maandamano ya Walibya ya kuupinga utawala wa Kizayuni

Kabla ya hatua hii ya Bunge la Libya; siku kadhaa zilizopita Bunge la Algeria pia lilipiga kura kwa asilimia mia moja na kumruhusu Rais wa nchi hiyo kuingia vitani na utawala wa Kizayuni kwa ajili ya kuwatetea na kuwaunga mkono wananchi wasio na hatia wa Palestina iwapo italazimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live