Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge la Libya laikabidhi UN sheria mpya za uchaguzi lilizozidhinisha

Bunge La Libya Bunge la Libya laikabidhi UN sheria mpya za uchaguzi lilizozidhinisha

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) umesema kwamba umepokea hati rasmi ya sheria za uchaguzi wa rais na bunge zilizoidhinishwa hivi karibuni na Baraza la Wawakilishi la Libya, au Bunge.

UNSMIL imesema hayo katika taarifa yake na kuandika: "Tunaheshimu maamuzi ya taasisi huru za Libya na utatuzi wa kitaifa na wa kisiasa wa masuala ya nchi hiyo."

Taarifa hiyo ya Umoja wa mataifa imesisitiza pia kwamba, hatua zote zinazochukuliwa inabidi zitekelezwe na ziheshimiwe ili kuhakikisha kunakuweko mchakato mzuri wa uchaguzi wa amani, endelevu, utulivu na usalama wa kudumu nchini Libya.

Timu hiyo ya Umoja wa Mataifa imetilia mkazo pia dhamira yake ya kushirikiana na pande zote husika ili kufikia maelewano ya kuunda serikali moja ya Libya yenye nguvu, umoja na mshikamano na kuongeza kuwa, Umoja wa Mataifa uutafanya upembuzi yakinifu kuhusu sheria hizo na kuwasilisha maoni yake kwa wananchi wa Libya. Bunge la Libya

Bunge kwa kauli moja liliidhinisha sheria hizo wakati wa kikao rasmi siku ya Jumatatu. Hata hivyo, Baraza Kuu la Serikali lenye makao yake makuu mjini Tripoli limezikataa sheria hizo mpya na kuamua kufuta uwakilishi wake wa 6+6 siku ya Jumatano.

Kamati ya wajumbe 6+6 ni ya pamoja ya kutunga sheria. Inaundwa na wajumbe sita kutoka Baraza Kuu la Serikali na wajumbe sita kutoka bungeni na ina jukumu la kutunga sheria kwa ajili ya uchaguzi ujao.

Libya ilishindwa kufanya uchaguzi mkuu mwezi Disemba 2021 kama ulivyopangwa awali kutokana na vyama vya nchi hiyio kushindwa kuelewana kuhusu sheria za uchaguzi.

Tangu ulipoangushwa kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011 hadi hivi sasa, Libya imekuwa ikijitahidi kufanya mabadiliko ya kidemokrasia lakini haijafanikiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live