Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge la Gambia kukutana kujadili vifo watoto 70 vya dawa ya kikohozi

Daaf4711 C84c 46a1 92ff 485f5ef696bc Bunge la Gambia kukutana kujadili vifo watoto 70 vya dawa ya kikohozi

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: Bbc

Bunge la Gambia litakutana katika kikao kisicho cha kawaida kujadili vifo vya watoto karibu 70 vilivyohusishwa na dawa za kikohozi zilizotengenezwa nchini India.

Watoto walipatikana na matatizo makubwa ya figo.

Kikao cha Jumatano katika bunge kitakuwa ni cha kwanza cha wabunge nchini humo tangu mkasa huo ulipotokea mapema mwezi huu.

Maafisa nchini Gambia walisema hakuna visa vipya zaidi, lakini kuna visa 82 vilivyopo na 12 walipona.

Vingi kati ya visa vilivyopo vinahusisha watoto wenye umri wa mwaka mmoja na miaka miwili.

Mashirika ya kiraia nchini humo yanaongeza shinikizo kwa mamlaka kuchukua hatua dhidi ya wale waliohusika na uagizaji wa madawa.

Maafisa wa afya na shirika la Msalaba Mwekundu wameanza awamu ya pili ya kuitisha dawa hizo za kikohozi ili zisitumike.

Uchunguzi wa polisi umebaini kuwa Shirika la udhibiti wa madawa lilianzishwa kufanya kipimo cha usalama wa madawa.

Rais Adama Barrow ameweka tume ya uchunguzi kuchunguza vifo hivyo.

Chanzo: Bbc