Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge la DRC lamchagua Vital Kamerhe kuwa spika

Bunge La DRC Lamchagua Vital Kamerhe Kuwa Spika Bunge la DRC lamchagua Vital Kamerhe kuwa spika

Thu, 23 May 2024 Chanzo: voa

Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilimchagua Vital Kamerhe, ambaye nyumba yake ilishambuliwa vibaya siku ya Jumapili, kuwa spika.

Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilimchagua Vital Kamerhe, ambaye nyumba yake ilishambuliwa vibaya siku ya Jumapili, kuwa spika katika kura iliyocheleweshwa, ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kuunda serikali miezi mitano baada ya uchaguzi wa rais.

Nafasi ya spika inamfanya Kamerhe, mshirika wa karibu wa Rais Felix Tshisekedi, kuwa mtu wa pili mwenye mamlaka katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.

Kati ya wabunge 407 waliopiga kura siku ya Jumatatu, 371 walipiga kura kumuunga mkono Kamerhe kugombea uspika. Wabunge pia walitazamiwa kuwapigia kura wagombea wa nyadhifa nyingine sita katika baraza kuu la bunge.

Chanzo: voa