Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge la Algeria lapitisha sheria kali inayominya uhuru vyombo vya habari

Bunge La Algeria Lapitisha Sheria Kali Inayominya Uhuru Vyombo Vya Habari Bunge la Algeria lapitisha sheria kali inayominya uhuru vyombo vya habari

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: Voa

Bunge la Algeria Alhamisi lilipitisha sheria inayominya zaidi uhuru wa vyombo vya habari katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini kwa kuweka sheria kali za umiliki wa vyombo vya habari na kuwazuia waandishi wa habari kulinda vyanzo vyao.

Sheria hiyo inapiga marufuku vyombo vya habari vya ndani kupokea ufadhili au msaada wa vifaa wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja kutoka nje, chini ya tishio la kufunguliwa mashtaka ya uhalifu ikiwemo faini ya hadi dola 15,000.

Inakubali kuwa siri ya kitaalamu ni haki, lakini inaruhusu mahakama kuwalamizisha waandishi wa habari kufichua vyanzo vyao.

Inapiga pia marufuku kwa watu wenye uraia pacha kumiliki vyombo vyote vya habari au sehemu ya vyombo hivyo, na waandishi wa habari wanaofanyia kazi vyombo vya habari vya kigeni bila kibali, wanaweza kutozwa faini ya dola 7,600.

Chanzo: Voa