Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge la Afrika Kusini latoa mwito wa kushinikizwa Israel iheshimu amri ya ICJ

Museveni Akutana Na Ramaphosa Kwenye Ziara Ya Afrika Kusini Bunge la Afrika Kusini latoa mwito wa kushinikizwa Israel iheshimu amri ya ICJ

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bunge la Afrika Kusini limekaribisha kwa furaha "uamuzi wa kihistoria" wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu kesi ya mauaji ya kimbari iliyofunguliwa na Afrika Kusini dhidi ya Israel, na limetoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuushinikiza utawala wa Kizayuni kuheshimu na kutekeleza kivitendo amri ya mahakama hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na bunge la Afrika Kusini jana jioni, lazima amri ya ICJ itekelezwe na ni jukumu la jamii ya kimataifa kuishinikiza Israel kuhesimu amri hiyo ya kujiepusha kufanya mauaji ya kimbari huko Ghaza.

Bunge la Afrika Kusini limeiita amri hiyo ya mahakama ya ICJ kuwa ni ushindi muhimu wa haki za binadamu na kuongeza kuwa, uamuzi huo unazidi kutia nguvu uhalali wa msimamo wa Afrika Kusini juu ya wajibu uwa kukomeshwa vita mara moja huko Ghaza.

Katika taarifa yake hiyo, Bunge la Afrika Kusini limeitaka Israel kuheshimu amri hiyo ya lazima na kusitisha vitendo vyote vya mauaji ya halaiki huko Ghaza na dhidi ya watu wa Palestina.

Israel inafanya mauaji ya kimbari na jinai kubwa kupindukia dhidi ya Wapalestina

Bunge pia limelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, baada ya kuarifiwa rasmi kuhusu agizo la ICJ na kwa mujibu wa sheria yake, kuhakikisha hatua za haraka zinachukuliwa kwa vile hakuna serikali au taifa lolote duniani lililoko juu ya sheria.

Tarehe 29 mwezi uliopita wa Disemba, 2023, Afrika Kusini iliwasilisha shauri kwa ICJ na kufungua kesi dhidi ya Israel, kutokana na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.

Jana Ijumaa, Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imeiamuru Israel iache vitendo vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina. Hata kama mahakama hiyo imekwepa kuiamuru Israel ikomeshe mara moja jinai zake dhidi ya Wapalestina lakini Bunge la Afrika Kusini linasema huo ni ushindi wa haki za binadamu kwani hii ni mara ya kwanza kufikiwa hatua kama hiyo dhidi ya Israel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live