Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge la Afrika Kusini lampiga marufuku Malema na wabunge wengine

Bunge La Afrika Kusini Lampiga Marufuku Malema Na Wabunge Wengine Bunge la Afrika Kusini lampiga marufuku Malema na wabunge wengine

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Kiongozi wa upinzani nchini Afrika Kusini Julius Malema na wabunge wengine watano wa chama chake cha Economic Freedom Fighters (EFF) Jumatano waliadhibiwa kwa kupigw amarufuku kuhudhuria vikao vya bunge kwa mwezi mmoja bila malipo .

Kamati ya mamlaka na marupurupu ya bunge iliwapata na hatia ya kudharau bunge kwa kuvamia jukwaa wakati wa hotuba ya Rais Cyril Ramaphosa kuhusu hali ya taifa mwezi Februari.

Spika kisha akasimamisha shughuli huku maaafisa wa usalama wakimwondoa Bw Malema na wabunge wengine nje ya ukumbi.

Kamati hiyo iliongeza kuwa "kila mjumbe lazima pia aombe radhi ana kwa ana katika Bunge kwa rais, spika na watu wa Afrika Kusini" kwa kuvuruga hotuba ya rais na "kuiweka nchi katika hali mbaya".

Chanzo: Bbc