Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge kujadili kashfa inayomkabili Rais Cyril Ramaphosa

 Bunge Kujadili Kashfa Inayomkabili Rais Cyril Ramaphosa Bunge kujadili kashfa inayomkabili Rais Cyril Ramaphosa

Tue, 13 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Hii ni kashfa inayomzunguka rais Ramaphosa ya madai ya kuficha wizi wa sarafu za kigeni katika shamba lake la kibinafsi mnamo 2020.

Bunge la Afrika Kusini linatarajiwa kufanya kikao maalum kushughulikia ripoti ya jopo la wataalam wa kisheria ambao wamegundua kuwa Rais Cyril Ramaphosa anaweza kuwa amevunja kiapo chake.

Hii ni kuhusiana na kashfa ya suala la shamba inayomzunguka rais, ambapo Bwana Ramaphosa ameshtakiwa kwa kuficha wizi wa sarafu za kigeni katika shamba lake la kibinafsi mnamo 2020.

Mwandishi wa BBC kutoka Johannesburg Nomsa Maseko anaripoti kwamba hatima ya Rais Cyril Ramaphosa itakuwa mikononi mwa wabunge wanapopiga kura kuhusu iwapo ataachishwa kazi.

Uthibitisho wa kufanya makosa baada ya madai kwamba alificha wizi wa sarafu za kigeni kutoka kwa shamba lake la kuwinda imechochea wito wa kujiuzulu kwake.

Hata hivyo, Bwana Ramaphosa amekanusha mara kwa mara makosa yoyote.

Chama cha ANC kilicho madarakani kimewaagiza wabunge wake 230, wakiwemo wale wanaojulikana kuwa wapinzani wa rais kukataa ripoti ambayo ilibaini kwamba huenda amevunja kiapo chake kwa sababu matokeo ya ripoti hiyo yanapingwa mahakamani.

Lakini baadhi yao wanaweza kukataa kufanya hivyo na kujiunga na vyama vya upinzani kwa ajili ya kupiga kura ya kutokuwa na imani naye na kuruhusu kuanza kwa kesi ya kufunguliwa mashtaka.

Ikiwa Bwana Ramaphosa ataepuka hili bungeni, inawezekana atachaguliwa tena kama rais wa ANC katika mkutano wa chama unaoanza Ijumaa.

Chanzo: Bbc