Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge Nigieria lagoma kununua boti ya kifahari ya Rais

Nigeria Yagoma Kununulia Boti Ya Kifahari Bunge Nigieria lagoma kununua boti ya kifahari ya Rais

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Wawakilishi nchini Nigeria, limeugomea mpango wa Serikali kununua boti ya kifahari (Yatch), kwa ajili ya matumizi ya Rais wa nchi hiyo, yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 6, sawa na makadilio ya Sh15 bilioni.

Hayo yamebainishwa jana Alhamisi 2, 2023; na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Matumizi, Abubakar Bichi, alipokuwa akizungumza na wanahabari baada ya kupitishwa kwa Muswada wa Matumizi ya Fedha wa 2023.

Bichi, ambaye ni mwanachama wa chama tawala cha Rais Tinubu, amesema wabunge hawakuwa tayari kupitisha bajeti kwa ajili ya boti hiyo na badala yake, wamehamisha fedha hizo (dola milioni 6) na kuziongeza katika bajeti ya mikopo ya wanafunzi.

“Hakuna bajeti kwa ajili ya manunuzi ya Yacht ya Rais, kwa sababu fedha hizo zimeongezwa kwenye bajeti ya mikopo kwa nafunzi ambao umeongezeka kutoka N5 bilioni hadi N10 bilioni,” amesema Mbunge Bichi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live