Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge Gambia lapinga mswada wa kuruhusu ukeketaji

Bunge Nchini Gambia Lapinga Mswada Wa Kuruhusu Ukeketaji.png Bunge Gambia lapinga mswada wa kuruhusu ukeketaji

Tue, 16 Jul 2024 Chanzo: Bbc

Wabunge nchini Gambia wamekataa mswada unaotaka kubatilisha marufuku ya mwaka 2015 ya ukeketaji.

Spika wa Bunge, Fabakary Tombong Jatta alisema wabunge wengi wamepiga kura dhidi ya mswada huo hata kabla ya kusomwa kwa mara ya tatu na mwisho, unaotarajiwa baadaye mwezi huu.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu na Umoja wa Mataifa yalikuwa yamewataka wabunge kuzuia mswada huo uliowasilishwa mwezi Machi baada ya shinikizo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa dini ya Kiislamu.

Gambia ni miongoni mwa nchi 10 zenye viwango vya juu vya ukeketaji, huku asilimia 73 ya wanawake na wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wakiwa wamefanyiwa utaratibu huo.

Mswada, uliowasilishwa na Almameh Gibba, ilikataliwa baada ya wabunge kupiga kura dhidi ya vifungu vyake vyote vilivyopendekezwa.

Bi Jatta alisema mswada huo "umekataliwa na mchakato wa kutunga sheria umekamilika", na kwa hivyo haungeweza kwenda hatua iliyofuata yaani kusomwa kwa mara ya tatu.

Ulipowasilishwa mwezi Machi, mswada huo uliidhinishwa na wabunge wengi, na hivyo kuongeza matarajio ya Gambia kuwa nchi ya kwanza kubatilisha marufuku ya tabia hiyo.

Katika utaratibu wa ukeketaji, unaofanywa Gambia mwanamke hukatwa ‘’kisimi’’,na kushonwa sehemu za siri ili asiweze kufanya au kufurahia tendo la ndoa.

Chanzo: Bbc