Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bukina Faso watangaza siku mbili za maombolezo vifo vya watu 41

Ae3d3003465250e7c0e47c0901380cda Bukina Faso watangaza siku mbili za maombolezo

Sun, 26 Dec 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Serikali ya Burkina Faso imetangaza siku mbili za maombolezo kuanzia Jumapili baada ya watu 41 kuuawa katika shambulio lililofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa wanajihadi kaskazini mwa nchi hiyo.

"Kazi ya msako katika eneo la mashambulizi ya kuvizia ya makundi ya kigaidi yenye silaha ... imesaidia kubaini idadi ya maiti 41. Rais ametoa amri ya maombolezo ya kitaifa ya saa 48,” imesema taarifa ya serikali iliyotolewa Jumamosi jioni.

Serikali ilisema waliofariki ni pamoja na askari wa kikosi rasmi cha ulinzi kinachojulikana kwa jina la Volunteers for the Defence of the Motherland (VDP), kilichoundwa kwa ajili ya kusaidia jeshi hilo.

Wafanyakazi wa kujitolea hupokea mafunzo ya siku 14 na kisha kutumwa kwenye doria na misheni ya ufuatiliaji, wakiwa na silaha nyepesi.

Miongoni mwa walioathirika na shambulio la Alhamisi ni Ladji Yoro, anayesadikiwa kuwa kiongozi wa VDP nchini Burkina Faso, taarifa hiyo ilisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz