Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Buhari arefusha safari yake London ili kupata matibabu ya meno

Buhari Arefusha Safari Yake London Ili Kupata Matibabu Ya Meno Buhari arefusha safari yake London ili kupata matibabu ya meno

Wed, 10 May 2023 Chanzo: Bbc

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameongeza muda wa kukaa London kwa wiki moja kwa matibabu ya meno, msaidizi wake amesema.

Awali rais huyo alikuwa amesafiri kwenda Uingereza wiki iliyopita kuhudhuria kutawazwa kwa Mfalme Charles III.

Alipangiwa kurejea Nigeria wiki hii lakini sasa atasalia "kwa amri ya daktari wake wa meno, ambaye ameanza kumhudumia".

"Mtaalamu anahitaji kuonana na rais katika siku nyingine tano kwa ajili ya utaratibu ambao tayari umeanza," msemaji wa rais Femi Adesina alisema katika taarifa iliyotolewa Jumanne usiku.

Kukaa kwa muda mrefu kwa rais huyo mjini London kumezua shutuma kutoka kwa baadhi ya Wanigeria, wanaosema kwamba anapaswa kuyapa kipaumbele masuala ya ndani na kushughulikia changamoto za usalama zinazoikabili nchi hiyo.

Bw Buhari amesafiri hadi Uingereza mara kadhaa katika kipindi chake cha urais kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi huku kukiwa na uvumi kuhusu afya yake. Ameratibiwa kumkabidhi Rais Mteule Bola Tinubu tarehe 29 Mei.

Chanzo: Bbc