Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Buhari afukuza wakuu wa vikosi vya jeshi

3851edd0bb53c522f00d5128af75ff27 Buhari afukuza wakuu wa vikosi vya jeshi

Thu, 28 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

RAIS wa Nigeria, Muhammadu Buhari amewafukuza kazi wakuu wa vikosi vya jeshi vya nchi hiyo ambao aliwateua wakati alipoingia madarakani mwaka 2015.

Kutokana na hatua hiyo, Rais Buhari alituma barua pepe ya majina ya waliowabadilishwa.

Inaelezwa kuwa mpaka sasa hakuna sababu iliyotolewa ya kufukuzwa kwa viongozi wa Jeshi la Wanamaji, Jeshi la Anga na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi.

Hatua hiyo imefanyika wakati Nigeria inaendelea kukabiliana na ukosefu wa usalama ulioenea ikiwa ni pamoja na uasi wa muda mrefu unaofanywa na kundi la Boko Haram na utekaji nyara uliokithiri.

Buhari, jenerali wa zamani wa jeshi alichaguliwa mwaka 2015 kwa ahadi ya kumaliza uasi katika Mkoa wa Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Hata hivyo, Boko Haram inaendelea kufanya mashambulio licha ya serikali mara kadhaa kueleza kuwa wapiganaji wa kiisilamu wameshindwa.

Chini ya uongozi wa Buhari, mapigano kati ya wakulima na wafugaji wa ng'ombe katika eneo la kati la nchi hiyo pia yamezidi kuwa mabaya na utekaji nyara Kaskazini Magharibi.

Chanzo: habarileo.co.tz