Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Brian Chira hakuwa shoga: Babu yake afunguka A-Z

Brian Chira Ok 11 Brian Chira.

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa TikToker maarufu nchini Kenya, Brian Chira, hakuwa shoga kama ambavyo mitandao iliripoti baada ya kifo chake kilichotokea mwezi uliopita. Babu yake Brian Chira amefunguka jinsi kifo cha kijana huyo kilivyoathiri familia yao.

Kwenye mahojiano aliyofanyiwa na Tuko, Babu wa Brian Chira anamkumbuka Brian kama kijana mtulivu, mkimya na aliyekuwa na ndoto kubwa ya kumiliki kituo chake cha utangazaji. Lakini ndoto na maono ya Chira yalibadilika na kufa mapema, baada ya kifo cha mama yake mkubwa aliyekuwa anamlea.

Kwa mujibu wa maelezo ya Babu, Brian Chira alipendwa sana na mama yake mkubwa aliyekuwa akimlipia ada ya shule na mahitaji yake yote muhimu. Kifo cha mama yake mkubwa kilimuathiri vibaya Brian, licha ya kupata msaada wa matunzo kutoka kwa Bibi yake.

“Maisha kwake hayakubadilika sana baada ya kifo cha mama yake, ada ililipwa, na alipelekwa shuleni isipokuwa kuna wakati alilazimika kusoma mbali na nyumbani, alikuwa kijana mtiifu, alitaka kuwa kiongozi.”

“Mama yake mkubwa alimtunza baada ya mama yake kufariki. Alimpeleka shule, hadi chuo kikuu, na kisha akafa, na shida zilianza kumpata Brian Chira. Mama yake mkubwa alikuwa tegemeo lake kubwa. Hakuwa sawa. Hapo ndipo unyonge ulipoanza. Aliona dunia imeisha. Lakini bibi yake alijitahidi kumlea.”

Kutokana na maelezo ya Babu wa Brian Chira, Babu huyo alikanusha madai kuwa Brian Chira alikuwa shoga, akidai aliona madai hayo mtandaoni na kwamba mjukuu wake hakuwahi kuzungumzia hali ya jinsia yake.

“Tulimfahamu kuwa ni mtu wa kukaa kimya, alikuwa anaongea kwa upole ungetaka aendelee kuongea, hakuwa na sauti ya juu, na tulimfahamu kuwa ni mtoto mzuri, tulishtuka kuwa ana tatizo la unywaji pombe.”

“Ni kitu ambacho sijawahi kusikia, hata kupitia vyombo vya habari, hata kutoka kwa Brian. Sijawahi kumsikia hata mara moja. Nilichosikia kutoka kwake ni, ‘Nataka kuwa msomi, mchumi, nataka kuanzisha kituo changu cha utangazaji’ lakini sikuwahi kusikia kitu hicho kutoka kwake.”

Aliwakashifu vikali wanamtandao walioshea picha za maiti ya Brian akiwataka kudumisha maadili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live