Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Breki zangu zilifeli,' asema dereva wa lori la Kenya

 'Breki Zangu Zilifeli,' Asema Dereva Wa Lori La Kenya 'Breki zangu zilifeli,' asema dereva wa lori la Kenya

Tue, 4 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Dereva wa lori lililoua watu 52 kwenye makutano ya barabara yenye shughuli nyingi magharibi mwa Kenya siku ya Ijumaa amesema breki kwenye gari zilifeli.

"Nilikanyaga breki lakini zilifeli, na sikuweza kulidhibiti," Gilbert Ntuyemungu, ambaye anatoka Rwanda, aliwaambia waandishi wa habari kutoka kwa kitanda chake hospitalini.

The driver says he remembers hearing people screaming and falling by the roadside - and after that he cannot recall much. He later found himself in hospital.

Dereva anasema anakumbuka kusikia watu wakipiga kelele na kuanguka kando ya barabara - na baada ya hapo hawezi kukumbuka mengi.

Baadaye alijikuta hospitalini.

Lori hilo lilikuwa likielekea Uganda kutoka kwa kampuni ya saruji ya Kenya lilipoingia kwenye magari ya abiria na wachuuzi kando ya barabara Ijumaa jioni.

Ajali hiyo ilihusisha magari tisa na pikipiki kadhaa.

Kamanda wa polisi wa eneo hilo Geoffrey Mayek aliambia BBC kwamba mara Bw Ntuyemungu atakapopata nafuu na kuruhusiwa kutoka hospitalini, maafisa walichukua taarifa na uchunguzi utabainisha iwapo atakabiliwa na mashtaka yoyote.

Chanzo: Bbc