Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking: Rais Zuma Ajisalimisha Polisi

Zuma?fit=1200%2C794&ssl=1 Breaking: Rais Zuma Ajisalimisha Polisi

Thu, 8 Jul 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Breaking: Rais Zuma Ajisalimisha Polisi July 8, 2021 by Global Publishers



Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amejisalimisha polisi kuanza kifungo cha miezi 15 jela baada ya kuhukumiwa kwa kosa la kudharau agizo la Mahakama.

Ripoti zinasema Zuma alikwenda polisi Jumatano usiku jana karibu na nyumbani kwake katika mkoa wa KwaZulu-Natal. Hii imekuja baada ya polisi kuonya kuwa, walikuwa tayari kumkamata kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 79 iwapo asingejisalimisha kwao kufikia siku ya Jumatano.

Bwana Zuma alihukumiwa kifungo hicho cha miezi 15 jela wiki iliyopita baada ya kukaidi agizo la Mahakama la kumtaka kutoa ushahidi kuhusu kesi ya ufisadi, wakati alipokuwa madarakani kwa miaka tisa.

Hukumu dhidi ya Zuma ambayo ni ya kwanza dhidi ya Rais wa nchi, ilizua mtafaruku wa kisheria nchini Afrika kusini, huku muda wa mwisho ukiwekwa wa kujisalimisha usiku wa jana wa kukamatwa kwake.



Muda huo uliwekwa baada ya Rais Zuma kukataa kujisalimisha mwenyewe siku ya Jumapili. Alishtakiwa kwa tuhuma za ufisadi katika kipindi cha miaka tisa ya uongozi wake madarakani. Tuhuma ambazo mwenyewe alizikana na kusema kuwa ni mhanga wa kisiasa.

Awali, rais huyo wa zamani alikuwa amesema hatajisalimisha Jumapili iliyopita, hatua iliyosababisha polisi kumpa hadi Jumatano usiku kufanya hivyo.

Binti yake Dudu Zuma-Sambudla, kwenye ukurasa wake wa Twitter, aliandika kuwa, baba yake alikuwa njiani kwenda jela, lakini alikuwa katika hali nzuri.

Hii ndio mara ya Kwanza raia wa Afrika Kusini wanashuhudia rais wao wa zamani akifungwa jela. Zuma aliwahi kufungwa jela wakati wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini mwake. 

Mwanasiasa huyo mwenye sifa ya ucheshi, aliondolewa madarakani na chama cha ANC baada ya kudaiwa kujihusisha na ufisadi, na nafasi yake kuchukuliwa na rais wa sasa Cyril Ramaphosa.

Rais huyo wa zamani anakabiliwa na mashtaka 16 ya ufisadi, kwa kuhusika na ununuzi wa silaha kutoka kampuni za kuuza silaha barani Ulaya. Baadhi ya wafuasi wake waliokuwa wamekusanyika nje ya nyumba yake walielezea kutofurahishwa na kiongozi wao huyo kuhukumiwa kifungo gerezani. 

Share this:TweetWhatsApp Related

Chanzo: globalpublishers.co.tz