Botswana inasema imeshuhudia ongezeko kubwa la uwindaji haramu wa faru, na kupoteza takriban theluthi ya idadi ya wanyama hao walio hatarini kutoweka.
Waziri wa Utalii, Philda Kereng, aliliambia bunge kuwa vifaru 138 waliuawa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, ingawa idadi ilipungua kwa kasi mwaka jana.
Takwimu rasmi zinasema ni wanyama wawili pekee waliowindwa katika kipindi cha miaka mitano hadi 2017.
Waziri huyo alihusisha kuongezeka kwa mahitaji ya kimataifa ya pembe za faru, haswa katika bara la Asia.
Pia alitoa mfano wa kuhama kwa magenge ya ujangili kutoka nchi nyingine za kusini mwa Afrika.
Wahifadhi wanakadiria Botswana ilikuwa na vifaru chini ya 400 mwaka 2019.