Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Boti yawaka moto, wahamiaji 14 wafariki

Capture Kkaka Boti yawaka moto, wahamiaji 14 wafariki

Wed, 29 Jun 2022 Chanzo: VOA

Takribani wahamiaji 14 wamefariki wakati boti waliokua wanasafiria iliposhika moto katika jimbo la kusini la Senegal la Kasamance.

Meya wa mji wa pwani wa Kafountine katika jimbo la Kasamance David Diatta ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumanne kwamba walifanikiwa kupata mili ya watu hao 14 baada ya tukio hilo la moto siku ya Jumatatu. Idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka aliongeza.

Muuguzi mkuu wa mji huo Bourama Faboure alisema kwamba watu 21 wamejeruhiwa wakiwemo wane waliopata majeraha ya moto. Boti hiyo ilikuwa imebeba kiasi cha watu 140 na takribani watu 90 kati yao walionusurika walitambuliwa.

Diatta alisema watu hao walikuwa raia kutoka nchini Guinea, Nigeria, Gambia na Senegal.

Chanzo: VOA