Mon, 10 Jul 2023
Chanzo: Bbc
Waokoaji wa Uhispania wapo katika maji ya nje ya Visiwa vya Canary kutafuta mashua iliyobeba wahamiaji wasiopungua 200 wa Kiafrika ambao walitoweka zaidi ya wiki moja iliyopita.
Kundi la misaada la Walking Borders linasema mashua hiyo ya wavuvi ilisafiri kutoka Kafountine, mji wa pwani kusini mwa Senegal ambao uko takriban kilomita 1,700 (maili 1,057) kutoka Tenerife.
Kundi hilo linasema watoto wengi wako kwenye boti hiyo, shirika la habari la Efe la Uhispania linaripoti.
Boti mbili sawia zilizobeba makumi ya watu zaidi pia zinasemekana kupotea.
Chanzo: Bbc