Boniface Mwangi amejiuzulu kama mwenyekiti wa chama cha Ukweli PartyMwangi ambaye pia ni mwanaharakati, ametangaza kwamba hatawania kiti chochote katika uchaguzi mkuu wa 2022Kulingana na Mwangi siasa za Kenya huamuliwa na pesa na ndio hupelekea wananchi kuwachagua viongozi wasiofaaMwangi ameapa kuendelea kupigania uhuru na haki za wananchiMwanaharakati Boniface Mwangi amejiuzulu kama mwenyekiti wa chama cha Ukweli Party na pia ametangaza kwamba hatawania kiti chochote katika uchaguzi mkuu wa 2022.
Chama hicho kwenye arafa yake Jumatano, Agosti 10 kilisema kwamba Mwangi aliomba ajiuzulu ili aweze kushughulikia masuala ya kifamilia.
" Tungependa kutangaza kwamba mwenyekiti wa chama chetu Boniface Mwangi ameomba ajiuzulu ili apata nafasi ya kuwa na familia yake," Arifa ya chama hicho ilisoma.
Chama hicho pia kilimpongeza kwa uongozi mzuri na kimemtakia heri njema anakoelekea.
Awali, Mwangi alikuwa ametangaza kwamba amejiondoa katika siasa za Kenya akidai zimekumbwa na udanganyifu na ulaghai mwingi.
" Kwa ajili ya kujipa fursa ya kupona na kupata amani moyoni, ningependa kusema kwamba sitawania kiti chochote katika uchaguzi mkuu wa 2022," Alisema Mwangi.