Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bomu lamjeruhi mwanaume Mrusi katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati

Bomu Lamjeruhi Mwanaume Mrusi Katika Jamuhuri Ya Afrika Ya Kati Bomu lamjeruhi mwanaume Mrusi katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Mkuu wa kituo cha utamaduni wa Urusi katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati amejeruhiwa kwa bomu la kifurushi.

Ubalozi wa Urusi umesema amejeruhiwa kichwani na anapata matibabu katika hospitali katika mji mkuu, Bangui.

Kikundi cha mamluki cha Urusi Wagner kiliilaumu Ufaransa kwa tukio hilo, likiishutumu kwa kudhamini ugaidi.

Kikundi cha Wagner kinaendesha harakati zake katika nchi kadhaa za Afrika zikiwemo Mali na Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Chanzo: Bbc