Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bomu lalipuka Equatorial Guinea, watu 20 wafariki

Download 7.jpeg Bomu lalipuka Equatorial Guinea, watu 20 wafariki

Mon, 8 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Watu 20 wamefariki dunia huku wengine zaidi ya 600 wakijeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliotokea nchini Equatorial Guinea jana jumapili.

Mlipuko huo umetokea karibu na kambi za wanajeshi mji mkuu wa Bata ambao ni maarufu kwa mafuta na gesi ukiwa na wakazi milioni 1.4

Rais wa Equitorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema amenukuliwa na mitandao mbali mbali akisema mlipuko huo umesababishwa na uzembe uliohusishwa na huifadhi baruti kali kambini.

Aliongeza kwamba huenda tukio hilo limetokea kufuatia hatua ya wakulima kuchoma mashamba yanayozunguka kambi za jeshi.

Naye Waziri wa Afya  wa nchi hiyo,  Colonel Remy Lamah kupitia mtandao wake wa Twitter anaomba  wahudumu wa afya kujitolea na kwenda katika hospitali ya eneo la Bata. Pia ametoa wito watu kujitolea kutoa damu kwa sababu ya idadi kubwa ya waliojeruhiwa

HAJI MANARA KAWASILI KUTOKA SUDAN “TUNAKWENDA KUCHUKUA UBINGWA”

Chanzo: millardayo.com