Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bomba la mafura laharibu mashamba, mto Niger Delta, Nigeria

Mafuta Shamba.jpeg Bomba la mafura laharibu mashamba, mto Niger Delta, Nigeria

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kusambaa mafuta kwa mara nyingine tena kutoka kituo cha Shell nchini Nigeria kumechafua mashamba na mto, na hivyo kukwamisha shughuli za maisha za wavuvi na wakulima katika jimbo la Niger Delta huko Nigeria, raia ambao kwa muda mrefu wamevumilia uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na sekta ya mafuta.

Wakala wa Taifa Unaohusika na Udhibiti wa Umwagikaji wa Mafuta Nigeria (NOSDRA) umeeleza kuwa mafuta hayo yamesambaa katika jamii hizo tajwa kutoka katika bomba la mafita la Trans-Niger linalosimamiwa na Kampuni ya Mafuta ya Shell ambalo hupita katika eneo la Eleme huko Ogoniland.

Wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakilalamikia shughuli za uchimbaji mafuta kwa miongo kadhaa sasa zinazofanywa na kampuni hiyo kubwa ya nishati yenye makao yake makuu London.

Ripoti zinasema kuwa kiasi cha mafuta kilichomwagika hakijabainishwa, lakini wanaharakati wamechapisha picha za ardhi iliyochafuliwa ya mashamba na sehemu za maji zilizoharibiwa na miale ya mafuta na samaki waliokufa kutokana na msambao wa mafuta hayo ghafi yenye kunata.

Msambao wa mafuta huko Ogoniland kutoka bomba la Shell Wanaharakati wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa wameutaja msambao huu wa mafuta huko Niger Delta kuwa mkubwa wa iana yake ingawa mafuta kutoka kampuni hiyo ya Shell yamekuwa yakimwagiga mara kwa mara katika eneo hilo kutokana na uharibifu na ukosefu wa matengenezo ya mabomba.

Fyneface Dumnamene mwanaharakati wa mazingira amesema msambao wa sasa wa mafuta huko Niger Delta ni mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa huko Ogoniland jimboni humo katika kipindi cha miaka 16 iliyopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live