Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Boko Haram yadai kuwateka wanafunzi wa Nigeria

D11e988b8e5615fbca25841b20d52a07 Boko Haram yadai kuwateka wanafunzi wa Nigeria

Wed, 16 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KUNDI la wanamgambo wa kigaidi la Boko Haram, limesema limehusika na utekaji nyara mamia ya wavulana wa shule katika Jimbo la Kaskazini Magharibi la Katsina State.

Kundi hilo limeelezea jinsi lilivyoendelea kutekeleza mashambulio hatari katika wiki za hivi karibuni.

Mamia ya wavulana wa Shule ya Upili ya Serikali ya Kankara katika Jimbo la Katsina, hawajulikani walipo baada ya shambulio dhidi yao lililotokea Ijumaa iliyopita.

Kwa mujibu wa Daily Nigerian, Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, alisema hayo katika ujumbe wa dakika nne uliorekodiwa na kundi lililotekeleza shambulio hilo.

Alieleza sababu za kufanya shambulio hilo na kufanya utekaji nyara kuwa ni "Kwa sababu elimu ya Magharibi inaenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu."

"Kilichofanyika Katsina ni hatua ya kunadi Uislamu na kupinga elimu inayoenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu kwani elimu ya Magharibi hairuhusiwi na Allah na Mtume wake," tovuti hiyo ilimnukuu Shekau akisema.

Tovuti hiyo aidha, ilisema Shekau hakutoa maelezo kuhusu shambulio hilo, idadi ya wanafunzi waliotekwa au kuthibitisha ripoti kuhusu majadiliano na serikali.

Chanzo: habarileo.co.tz