Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Boko Haram waua watu 81 Nigeria

Boko Haram 3d71f Boko Haram waua watu 81 Nigeria

Wed, 4 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu 81 wameuawa na wengine hawajulikani walipo baada ya shambulizi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, mamlaka ya eneo hilo iliambia Agence France Presse Jumanne, Septemba 3, ikilishutumu kundi la wanajihadi la Boko Haram.

Kwa mujibu wa Polisi wa Jimbo la Yobe, karibu watu 150 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Boko Haram walishambulia kijiji cha Mafa siku ya Jumapili, Septemba 1, mwendo wa saa kumi jioni, wakiwa na silaha za moto na guruneti.

Miili 15 ilikuwa tayari imezikwa na jamaa zao wakati askari walipofika kutoa miili hiyo. Na idadi isiyojulikana ya waliouawa kutoka vijiji jirani, katika shambulio hilo, walichukuliwa na kuzikwa na jamaa zao kabla ya kuwasili kwa askari.

Polisi bado hawajatoa taarifa. Lakini mamlaka inaamini kwamba Boko Haram waliua watu wengi na kuchoma maduka na nyumba nyingi wakati wa shambulio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live