Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya mikopo yatakiwa kutoa mikopo vyuo vikifunguliwa

KANALI.webp SADC: Usafirishaji bidhaa uendelee licha ya corona

Fri, 29 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAOFISA waandamizi na makatibu wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), wamependekeza kuruhusu biashara za bidhaa zote kuendelea kusafirishwa katika nchi zao kama ilivyokuwa kabla ya janga la virusi vya corona.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa ngazi ya makatibu wakuu uliofanyika kwa njia ya mtandao juzi jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert Ibuge, alisema mkutano huo umejadili na kutoa mapendekezo ya kuondoa vikwazo vyote vya kibiashara ili kuendeleza uchumi ndani ya jumuiya.

Balozi Ibuge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Makatibu Wakuu, alisema kuwa uamuzi huo utawawezesha wananchi kuendelea na maisha yao ya kawaida na biashara zao kwa kuwa janga la corona litaendelea kuwapo kwa muda ambao ukomo wake haujulikani japo juhudi za kuukabili ugonjwa huo zinaendelea.

“Kikao cha makatibu wakuu cha leo (juzi), kimependekeza kuondoa kikwazo cha bidhaa mahususi tu kupita katika mipaka yetu badala yake bidhaa zote zinazowezesha wananchi wetu kuendelea na maisha, ni lazima ziruhusiwe kupita katika mipaka ya nchi wanachama wa SADC," alisema.

Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa ni muhimu wa wanaSADC kujumuika katika wakati huu na kuona ni jinsi gani wanaweza kushirikiana na kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi wanachama wa SADC unakua kwa kuongeza juhudi katika sekta ya biashara.

Balozi Ibuge alifafanua: Kwa mfano halisi sisi kama Tanzania hatukufunga mipaka yetu, na katika kutokufunga mipaka yetu, bado tunatambua kwamba tunaendelea kuwategemea wenzetu kama wanavyotutegemea sisi.

"Tuna bandari inayohudumia nchi nane za SADC na zisizokuwa za SADC na ambazo ndizo hasa tunapozungumzia utengamano na mazingiara ya kufanya biashara na kuzingatia tahadhari mbalimbali za uonjwa wa Covid-19 ambazo nchi hizo zimekuwa zikichukua."

Alisema mkutano huo pia ulijadili hali ya kifedha ndani ya jumuiya, utekelezaji wa maazimio yaliyotokana na kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC ambayo ni menejimenti ya maafa, utekelezaji wa kaulimbiu ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC isemayo 'Mazingira Wezeshi kwa Ajili ya Maendeleo Endelevu na Jumuishi ya Viwanda, Kukuza Biashara na Ajira Ndani ya SADC' na mapitio ya hali halisi ya biashara baina ya nchi.

Alisema viongozi hao pia walijadili maendeleo ya viwanda ndani ya jumuiya na taarifa ya utekelezaji wa Mkakati wa Maendeleo ya Viwanda wa Jumuiya na mpango kazi wake.

Mkutano huo ulihusisha wataalamu kutoka nchi wanachama 12 wa SADC kutoka sekta za mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, fedha na mipango, uchukuzi na mawasiliano, viwanda na biashara, maliasili na utalii pamoja na afya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live