Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Utalii Afrika Kusini kuvunjwa mzozo wa udhamini wa Tottenham

Bodi Ya Utalii Afrika Kusini Kuvunjwa Mzozo Wa Udhamini Wa Tottenham Bodi ya Utalii Afrika Kusini kuvunjwa mzozo wa udhamini wa Tottenham

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya utalii ya Afrika Kusini inatazamiwa kuvunjika kutokana na mzozo kuhusu mapendekezo ya ufadhili wa klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza Tottenham Spurs, ripoti ya vyombo vya habari nchini humo imeeleza.

Mkataba huo ulitupiliwa mbali mwezi uliopita kufuatia ghasia hasa kutoka kwa mashirikisho ya kitaifa ya michezo na vyama vya wafanyikazi vilivyo na uhaba wa pesa, ambao wanaamini kuwa pesa hizo zingetumiwa vyema mahali pengine.

Mkataba wa miaka mitatu wa udhamini shati ulikuwa na thamani ya takribani dola milioni 51.

"Katika hali zote, ninaamini kuwa kuna sababu nzuri ya kuvunja bodi na nitafanya hivyo rasmi kupitia gazeti la serikali mnamo Ijumaa 21 Aprili 2023," Waziri wa Utalii Patricia de Lille alinukuliwa akisema.

Timu ya watu watatu inatarajiwa kuchukua majukumu ya bodi hiyo ikisubiri uteuzi wa bodi mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live