Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodaboda, baiskeli zapigwa 'stop' kuingia mjini

Boda Mjini Bodaboda, baiskeli zapigwa 'stop' kuingia mjini

Tue, 22 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Burundi imeanza kutekeleza marufuku ya usafiri wa bodaboda, pikipiki na baskeli katikati mwa jiji la Bujumbura.

Tangu usiku wa manane polisi wanapiga doria kwenye maeneo ya vitongoji vya jiji kuzuwia kusikuwepo na atakayekiuka hatua hiyo. Hali hiyo imesababisha msongamano mkubwa kwenye vituo vya mabasi, huku baadhi ya raia wakiamua kuelekea kwenye shuhuli zao kwa mguu.

Kaskazini kama magharibi mwa jiji la Bujumbura nimeshuhudia hatua hiyo ya waziri wa mambo ya ndani, maendeleo ya jamii na usalama Gervais Ndirakoca, ya kupiga marufu bodaboda, Pikipiki na baskeli kuingia mjini kati imeheshimishwa.

Baadhi ya raia nimeshuhudia wakibeba mizigo kichwani, na kutembea kwa mguu. Huku wengine walosubiri mabasi katika mitaa ya kaskazini mwa jiji wamelalamika ya kuwa kupigwa marufu bodaboda, Pikipiki na baskeli kumewasababishia usumbufu mkubwa.

"Nilikuwa nikitumia piki piki ama baskeli ili niweze kufika kwenye, eneo langu la shuhuli, lakini sasa naona raia tutaabika kweli. Itakuwa vigumu kufika kazini kwa wakati unaofaa. Hii ni hatari kwa kweli," amesema abiria mmoja ambaye hutumia bodaboda.

Mtumiaji mwengine pia ameelezea wasiwasi wake akisema "hali inaelekea kuwa ngumu, mimi nilikuwa nikitumia usafiri wa piki piki nanunuwa daga kwenye soko ya cotebu na kwenda kuziuza mtaani Gasenyi. Sina uwezo mkubwa wa kukodi gari hivyo kazi yangu naona imeharibika."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live