Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodaboda anayefanana na Wajackoyah, wateja wamkimbia

WAJA OWI Bodaboda anayefanana na Wajackoyah, wateja wamkimbia

Fri, 29 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gordon Owino, jamaa mwendesha boda boda amabye umaarufu wake umekuja baada ya kugundulika kwamba anafanana na mgombea urais kwa Chama cha Roots, wakili msomi George Wajackoyah amefunguka mengi jinsi amabvyo maisha yake yamebadilika tangu wimbi hilo la kumfananisha na Wajackoyah limkute.

Akizungumza kwenye mahojiano ya kipekee na kituo kimoja cha habari ya mitandaoni nchini humo, Owino amesema kwamba umaarufu huo umeingilia kazi yake sana kwani tangu akutanishwe na Wajackoyah sasa kila mtu anamuona kama mtu maarufu ambaye ametajirika na hilo limeporomosha kazi yake ya bodaboda.

“Umaarufu huo umeniathiri pakubwa sana kwa sababu nilikuwa na watu ambao walikuwa wateja wangu wa bodaboda lakini sasa wananiona kama supastaa sana na badala ya kubeba abiria niwapeleke, wao wanazingatia sana huo umaarufu ambao niko nao.

“Watu wanataka kupiga picha na mimi, wengine wanataka kunihoji, wengine wanataka nionekane kwenye chaneli zao, ni kitu kibaya na mwisho wa siku mimi mwenyewe huwa sipati faida. Nimepoteza vitu vingi nimeporomoka kiuchumi, hata kifedha kwa sababu ya hilo,” Owino alisema.

Alisema sasa watu popote aendapo wanamuona wanaanza kusema ndio huyo Wajackoyah na kuanza kumzingira jambao ambalo alisema si nzuri kwa upande wa riziki yake. Anasema imefikia mahali watu wanamuona wanaanza kumhusisha na bangi ambayo ndio ajenda kuu katika Ilani ya msomi wakili Wajackoyah.

Alisema kwamba familia yake pamoja na yeye mwenyewe ni Wakristo walokole na hata siku moja katika maisha yake hajawahi kugusa au hata kuonja bangi lakini tu kutokana na mfanano wake na Wajackoyah basi watu wanamuona tu kama mtumizi wa dawa hiyo ya kulevya.

Wiki jana, mtengeneza maudhui wa YouTube, mchekeshaji 2mbili alimkutanisha Owino na Wajackoyah katika ofisi yake katika kile kilionekana kuwa ni mshangao mkubwa kwa mgombea huyo wa urais. Wajackoyah alifurahi kumuona Owino na akamkabidhi saa yake ghali ya mkononi pamoja na kiasi cha pesa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live