Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodaboda Aliyeokota Mil 115 Akazirejesha kwa Mwenyewe Ageuka Milionea

LIBERIA BODA Rais Weah alipokutana na Toule.

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KIJANA anayeendesha bodaboda Liberia amekuwa shujaa wa kitaifa baada ya kuokota dola 50,000 (Tsh 115) ambazo zilikuwa zimepotea za mwanamke mmoja ambaye ni mfanyabiashara maarufu kaskazini mashariki mwa mpaka wa Ivory Coast.

Kijana huyo mdogo, Emmanuel Tolue (18), alizikuta pesa zikiwa kwenye mfuko wa plastiki barabarani na alisikia tangazo kwenye radio ambapo mwenye fedha Musu Yancy,aliomba sana atakayeziona amsaidie kwa kumrudishia..

Kijana huyo alimjulisha kuwa amezipata katika ofisi za serikali ya mitaa. Bi Yancy amesema kuwa amemzawadia Tsh milioni 22.8 pamoja na zawadi nyingine.

Mwanamke huyo alifurahi sana kupata taarifa ya kuwa anazipata pesa zake, alipiga kelele kumsifu Mungu mpaka sauti ilikuwa inakaribia kupotea.

Watu wengi walimsifia kijana huyo kwa kufanya usamaria mwema wa aina hiyo. Jambo kama hilo la ambalo kijana wa bodaboda amelifanya si jambo la kawaida kutokea Liberia, mara baada ya vita.

Aidha, Rais wa Liberia, George Weah amempa zawadi ya pikipiki mbili kijana huyo, dola 10,000 (Tsh milioni 23) na Scholarship ya kwenda kusoma nchi yoyote duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live