Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bobi Wine azuiwa kwa kukiuka masharti ya corona

152ec47b7a73bf7e3f283480065892a9 Bobi Wine azuiwa kwa kukiuka masharti ya corona

Sun, 10 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKATI siku zikizidi kuyoyoma kuelekea uchaguzi mkuu, mwanasiasa na mwanamuziki maarufu, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine mambo yanazidi kumwendea kombo kutokana na kuzuiwa na Jeshi la Polisi kuendelea na kampeni zake kutokana na kukiuka masharti ya corona.

Polisi wamesema Bobi Wine amekiuka masharti ya kufanya kampeni kutokana na kutozingatia masharti yaliyotolewa na serikali ya kudhibiti kuendelea kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona.

Mbali na maeneo yaliyofungiwa kufanyika kampeni kabisa, kila mgombea anatakiwa kuzingatia kanuni za afya mahali popote alipo ili kuwakinga wananchi na maambukizi ya virusi hivyo hatari.

Baada ya kuzuiwa kufanya kampeni, mwanasiasa huyo alirejeshwa nyumbani kwake Magere katika mji mkuu Kampala chini ya ulinzi mkali wa polisi.

Polisi wanamlaumu kwa kukiuka sheria za kupambana na janga la covid-19 na kukanusha kuwa wanamkamata kwa sababu za kisiasa.

"Mgombea huyo alishikiliwa kwa kuendelea kuandaa mikutano mikubwa wakati nchi inakabiliwa na tishio hatari la janga la covid-19 kwa kupuuza maagizo ya Tume ya Uchaguzi na Wizara ya Afya," ilisema sehemu ya taarifa ya Jeshi la Polisi.

Tukio hilo lilitokea katika wilaya ya Kalangala kwenye kisiwa cha Bugala Kaskazini mwa Ziwa Victoria moja ya maeneo ambayo kampeni zimepigwa marufuku kutokana na maambukizi ya virusi vya corona kuwa mengi.

Chanzo: habarileo.co.tz