Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bobi Wine awasilisha rufaa kupinga ushindi wa Museveni

E79293b3f9e0f12f74bc158242fcba13 Bobi Wine awasilisha rufaa kupinga ushindi wa Museveni

Wed, 10 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Aliyekuwa mgombea urais wa chama cha upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi amewasilisha rufaa iliyorekebishwa mahakamani kama hatua ya kuzidisha uzito wa ushahidi wake kupinga kisheria ushindi wa Rais Yoweri Museveni.

Sambamba na hilo upande wa Rais Museveni umepinga hatua ya kurekebisha shauri hilo ambalo mahakama ya juu inatakiwa kushungulikia na kutoa maamuzi yake kabla ya mwezi Mei ambapo rais mteule anatakiwa kuapishwa.

Kiongoz wa timu ya mawakili wa ‘Bobi Wine’ Medard Seggona amesema wamelazimika kuirekebisha rufaa waliyowasilisha baada ya kutatizwa katika mchakato wao wa kuandaa ushahidi wao wakati mteja wao alipokuwa amewekwa kizuizini nyumbani kwake

Tume ya Uchaguzi ya Uganda pamoja na mawakili wa Rais Museveni wamepinga kurekebishwa kwa rufaa hiyo. Wametoa angalizo kuwa hatua ya upande wa Kyagulanyi kutaka kuongezea ushahidi ili kuonyesha kuwa sheria fulani za uchaguzi zilikiukwa ni suala ambalo hawakubaliani nalo.

Chanzo: habarileo.co.tz