Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bobi Wine ataka amani Uganda

8a96bf594665e6d5c1f870096984de7c Bobi Wine ataka amani Uganda

Thu, 11 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Uganda, Robort Kyagulanyi “Bobi Wine’ amewataka waandamanaji ambao ni wafuasi wake kuacha vitendo vyovyote vinavyoweza kuashiria uvunjivu wa amani na kukubali yaishe baada ya miezi miwili iliyopita Yoweri Museveni kutangazwa mshindi wa kiti cha urais.

“Nawataka wote tutangulize amani mbele silaha na uonyeshe dhidi ya serikali ambayo imetuonea.” Alisema Bobi Wine akiwa katika Jukwaa la Umoja wa Kitaifa katika mji mkuu, Kampala.

Bobi Wine 39 alikuwa akizungumza kando ya meza iliyojaa faili, ambazo alidai zilikuwa na fomu za matokeo kutoka katika vituo vya kupigia kura, alisema karatasi hizo zinaonyesha matokeo ya kila kituo ambapo alidai kuwa 54%

Museveni hapo awali ameelezea uchaguzi wa Januari 14 kama uchaguzi "usio na udanganyifu" katika historia ya Uganda. Kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo, Museveni alishinda uchaguzi tena kwa zaidi ya asilimia 58 ya kura, wakati Bobi Wine akishika nafasi ya pili kwa karibu 35%

Chanzo: www.habarileo.co.tz