Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bobi Wine ashinda viti 41 vya Umeya, Museveni apoteza

Mtanzanianews 140651304 614587659329175 3031018638145228323 N 660x400 Bobi Wine ashinda viti 41 vya Umeya, Museveni apoteza

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Chama cha National Unity Platform (NUP) kinachoongozwa na Robert Kyagulanyi ‘Bobi Wine’, kimekishinda mbali Chama cha Rais Yoweri Museveni cha National Resistance Movement (NRM) katika chaguzi za Kampala Capital City Authority (KCCA).

Kwa mujibu wa Gazeti la The Independent, NUP kilishinda viti 41 dhidi ya 44 vya umeya na hivyo kukiacha mbali chama tawala. Viti vitatu vilivyosalia vilinyakuliwa na chama kinachohusiana na mgombeaji wa zamani wa urais Kizza Besigye, Forum for Democratic Change (FDC).

Hii ilikuwa mara ya kwanza katika historia kwa chama kinachoongozwa na Rais Museveni, NRM na Democratic Party (DP) kushindwa katika uchaguzi wa umeya Kampala.

Chama cha Wine pia kilishinda viti vyote vya ubunge kando na kiti cha Kampala ambacho kilitwaliwa na Mohamed Nsereko ambaye alikuwa mgombea huru.

Chanzo: millardayo.com