Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bobi Wine apeleka ombi mahakamani la kuwa huru

6fba211a0adb3167b75df4bb335395de Bobi Wine apeleka ombi mahakamani la kuwa huru

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WANASHERIA wa Aliyekuwa Mgombea wa Urais nchini Uganda kupitia Chama cha ‘National Unity Platform’ (NUP), Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine wamesema kuwa wamepeleka maombi ya kuachiwa huru kwake kwenye Mahakama Kuu, jijini Kampala, Uganda.

Kwa mujibu wa mwanasheria wa Bobi Wine, Anthony Wameri amesema kuwa mwanasiasa huyo alikuwa na njaa kwa kuwa watendaji wa ulinzi walikataza mtu yeyote kuingia nyumbani kwake tangia wiki iliyopita.

Taarifa zinasema nyumba ya Bobi wine imezungukwa na askari wa usalama waliowekwa ili kuzuia harakati zake kufuatia polisi wa ujasusi kupokea angalizo la kuzuka kwa ghasia na maandamano yaliyopangwa nchi nzima, kulingana na msemaji wa chama cha NUP, Fred Enanga.

Kyagulanyi na mke wake Barbra Itungo, wamewekwa chini ya ulinzi nyumbani kwao na vyombo vya ulinzi ikiwemo askari wa jeshi la UPDF na Jeshi la polisi nchini humo.

Chanzo: habarileo.co.tz