Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bobi Wine alia ushindi wa Museveni Uganda

31ffc71d425ac6d59d0e9621ef0a6aa8 Bobi Wine alia ushindi wa Museveni Uganda

Mon, 18 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

RAIS wa Uganda Yoweri Museveni amechaguliwa kuiongoza tena nchi hiyo kwa miaka mingine mitano, huku msindani wake wa karibu, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine akidai hatua ya serikali kuzima huduma za mitandao ilitoa mwanya wa kuibwa kwa kura.

Katika uchaguzi mkuu wa hivi karibuni nchini Uganda, Museveni alipata ushindi wa asilimia 59 dhidi ya Kyagulanyi aliyepata asilimia 35.

Ushindi wa Museveni ambaye ameliongoza taifa hilo kwa miaka 35 ulitangazwa na Tume ya Uchaguzi wa nchi hiyo.

Ushindi huo wa Museveni umepingwa vikali na Bobi Wine aliyedai kuwa hatua ya serikali ya kuzima huduma ya mtandao ilitoa mwanya wa kuibwa kwa kura.

Rais Museveni amesema hatavumilia mtu yeyote atakayejaribu kuhatarisha amani baada ya uchaguzi.

Kitendo cha kuzimwa kwa huduma hiyo ya mtandao pia kilipingwa vikali na wasimamizi wa uchaguzi waliosema kiliathiri utendaji kazi wao.

Aidha, Bobi Wine alibainisha kuwa kati ya vitendo ambavyo vimechangia kushindwa kwake, ni pamoja na zuio la kutoka nje ya nyumba yake lililowekwa na wanajeshi.

Alisema: ”Mbali na kukatisha huduma za mtandao, lakini mimi na mke wangu tulizuiliwa kutoka nje ya nyumba huku waandishi wa habari wa ndani ya Uganda na hata wale wa kimataifa pia wakizuiliwa kunifikia”.

Bobi Wine alibainisha kuwa, kumekuwa na machafuko na polisi kusababisha viofo kwa watu wengi, lakini pia wafuasi wake walinyanyaswa kwa amri ya serikali.

Ushindi huo wa juzi wa Museveni unamweka madarakani kwa awamu nyingine ya sita tangu kuingia madarakani mwaka 1986, kwa sasa ana miaka 76 huku akijinadi kuwa ataingoza nchi hiyo kwa uwezo mkubwa na kuiimarisha zaidi.

Chanzo: habarileo.co.tz