Mgombea wa urais nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, ameahirisha kampeni zake, kufuatia kujeruhiwa kwa maafisa wake wa kampeni na kuharibiwa kwa gari lake.
Kiongozi huyo wa upinzani anasema risasi zilifyatuliwa kwenye gari lake na kutoboa matairi ya gari lake na kumfanya asiweze kusafiri tena.
Video zilizosambazwa na timu yake ya kampeni kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha kitu ambacho hakikutambuliwa kikilipuka umbali wa mita kadhaa kutoka mahali alipokuwa.
Awali katika eneo la Kayunga, mashariki mwa Kampala, gesi za kutoa machozi zilitumika kuwatawanya wafuasi wake.
Maafisa wanne wa kampeni yake walijeruhiwa. Mmoja wao, aliyetambuliwa kama producer Dan Magic alipigwa usoni, mmoja wa Polisi wanaowalinda wagombea wa urais waliotolewa na Tume ya Uchaguzi pia alijeruhiwa.
“HUYU MTOENI ASIRUDI” MKURUGENZI ALIEMDHARAU WAZIRI MKUU ATUMBULIWA PAPO HAPO