Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bob Wine akamatwa baada ya kurudisha fomu

F6f1896b01928a8f0ff0d3845ef06e9c Bob Wine akamatwa baada ya kurudisha fomu

Tue, 3 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Mgombea urais wa Uganda kupitia Chama Cha ‘National Unity Platform’ (NUP) Robert Kyagulanyi maarufu kama ‘Bob Wine’ amekamatwa na polisi muda mfupi wakati akihutubia wananchi katika jiji Kampala nchini Uganda.

Taarifa kutoka katika kituo cha habari cha NTV nchini Uganda zinaeleza kuwa gari lake limeharibiwa na polisi. Mapema leo ‘Bob Wine’ aliwasili katika kituo cha uteuzi kilichopo Kyambogo Kampala kwa ajili ya kurudisha fomu ya kugombea urais.

Kutokana na wingi wa wafuasi wa mgombea huyo ambao ungeweka kuleta vurugu, polisi walitumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wafuasi hao. Hadi sasa, wagombea 10 wanawania nafasi hiyo wakiwemo kamanda wa zamani wa jeshi Jenerali Mugisha Muntu na aliyekuwa Waziri wa Usalama Jenerali Henry Tumukunde.

Wakati huo huo mmoja wa mgombea urais Patrick Amuriat kutoka chama cha 'Forum for Democratic Change' (FDC) anashikiliwa na polisi jijini kampala mara baada ya kukaidi amri ya idadi ya watu wanaotakiwa kumsindikiza wakati wa kurudisha fomu ya uteuzi.

Chanzo: habarileo.co.tz