Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Boakai aahidi kupambana na ufisadi

Boakai Liberiaaa.png Boakai aahidi kupambana na ufisadi

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais mpya wa Liberia Joseph Boakai ameahidi kupambana na ufisadi katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika baada ya kuapishwa jana kuiongoza nchi hiyo kufuatia kuibuka mshindi katika uchaguzi wa rais akimshinda mpinzani wake nyota wa zamani wa soka George Weah.

Boakai aliye na umri wa miaka 79 alimshinda Weah kwa kura chache mshindi wa zamani wa Ballon d'Or katika uchaguzi wa marudio wa Novemba mwaka jana kuwa kupata asilimia 50.64 ya kura dhidi ya asilimia 49.36 za mpinzani wake huyo. Akihutubia katika hafla ya kuapishwa, Rais mpya wa Liberia amesema na hapa ninamnukuu:" Tunaona nyakati ngumu, tunaona hakuna utendaji mzuri, tunaona ufisadi katika maeneo ya juu na ya chini,mwisho wa kunukuu."

Joseph Boakai ambaye umri na afya yake imeibua mijadala mingi huko Liberia jana ilimbidi kukatisha hotuba yake kwa muda kufuatia joto kali lililomuathiri. Rais mpya wa Liberia amesisitiza kuwa kuna haja ya kuijenga upya miundombinu, kuboresha huduma za msingi kwa wananchi na kuhakikisha kuwa Waliberia wanapatiwa fursa sawa za kimaendeleo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live