Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken kuanzia leo anafanya ziara katika mataifa manne ya bara Afrika, kuimarisisha uhusiano wa nchi yake na mataifa hayo kwenye nyanja mbalimbali.
Nchi ya Kwanza, atakayozuru Blinken ni Cape Verde, nchi ambayo kwa macho ya Marekani ni mfano mzuri wa nchi inayodumisha demokrasia barani Afrika.
Baadaye atakwenda nchini Cote Dvoire, Nigeria na hatimaye Angola, katika ziara inaelezwa ni kuimarisha zaidi ushawishi wa Marekani kwa nchi hizi, kisiasa, kiuchumi na kidiplomasia.
Ripot zinasema kuwa, katika ziara yake nchini Nigeria, makao makuu ya Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magahribi ECOWAS, Blinken atajadili hali ya usalama na kisiasa katika nchi za Niger, Mali na Burkina Faso ambazo zinaongozwa na jeshi.
Jumuiya ya ECOWAS imeendelea kupokea uungwaji mkono mkubwa kuhusu namna ya kutatua mzozo wa Niger tangu mwaka uliopita.